TSH BIL 800 KUONGEZA SUKARI NCHINI.

 

TSH BIL 800 KUONGEZA SUKARI NCHINI.

TSH BIL 800 KUONGEZA SUKARI NCHINI.

MOROGORO
Serikali imewahakikishia wananchi kuwa miradi inayoendelea ya upanuzi wa viwanda vya sukari nchini itachangia kwa kiasi kikubwa kujiendesha kwa ukamilifu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa upanuzi wa kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro Agosti 4 Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameeleza matumaini yake katika uwekezaji huo ambao umetumia kiasi cha shilingi bilioni  800 huku ukitarajiwa kuongeza kasi ya upatikanaji wa sukari nchini.
“Upanuzi wa kiwanda hiki una faida kubwa ikiwa ni pamoja na kulinda fedha zetu za kigeni, ambazo zingeweza kutumika kuagiza sukari nje ya nchi ili kukabiliana na uhaba wake. Uwekezaji wa mageuzi pia 
Mradi wa upanuzi wa kiwanda cha sukari kilombero  hadi sasa umefikia 83% ya utekelezaji  na utakapokamilika juni 2025 unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 za sasa hadi takriban tani 272,000
Miradi ya upanuzi viwanda vya sukari  inafanyika pia katika makampuni mengine yanayozalisha sukari nchini ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Mkulazi Holding, Mtibwa Sugar Estates, hii yote ikiwa inalenga kuhakikisha Tanzania inapata uwezo wa kujitosheleza kwa sukari.