JOZI 3,028,700 ZA VIATU ZAZALISHWA NCHINI
TANZANIA
Katika mwaka 2023/2024 jumla ya jozi za viatu 3,028,700 zimezalishwa nchini ikilinganishwa na jozi 2,927,500 zilizozalishwa mwaka 2022/2023.
Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) 151 wanaotengeneza bidhaa za ngozi pamoja na ongezeko la upatikanaji wa ngozi bora.