TSH BIL 18 KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KIBAMBA
DAR ES SALAAM
Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 18 kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa majisafi ambayo itaenda kuhudumia wakazi takribani 144,000 kutoka katika kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Utekelezaji wa mradi huu ni agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawatua ndoo kichwani Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.