TSH BIL 13 KUIBORESHA DUCE
DAR ES SALAAM
Mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 13 umesaniniwa kati ya serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) na Kampuni ya Shanxi kwa ajili ya ujenzi wa majengo mawili ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (The Dar es Salaam University College of Education -DUCE).
Majengo hayo mawili yatayojengwa ni majengo yatakayochukua Kitivo cha Binadamu na Sayansi ya Jamii, huku lingine likiwa ni jengo la uzamili na mkataba huo utatekelezwa ndani ya miezi 15 tangu kusainiwa mwezi Agosti 2024
Jengo la Uzamili litakuwa na maabara za kisasa za sayansi muhimu kwa utafiti na kujifunza kwa vitendo na muhimu zaidi, moja ya sakafu ya jengo hili itakuwa maalum kwa ajili ya kuchukua wanafunzi na wafanyakazi wenye mahitaji maalum.
"Kwa jengo la Sayansi ya Kibinadamu na Sayansi ya Jamii, litakuwa na aina ya ofisi za watumishi, vyumba vya mihadhara na semina ambavyo vitaboresha sana shughuli za ujifunzaji na ufundishaji.
KUMBUKA:- Hii ni mara ya kwanza kwa DUCE kupata ufadhili huo mkubwa kutoka kwa serikali wa kujenga majengo hayo mawili pamoja na kukarabati yaliyopo.