DKT SAMIA APONGEZWA KUIMARISHA BIASHARA

 

DKT SAMIA APONGEZWA KUIMARISHA BIASHARA

DKT SAMIA APONGEZWA KUIMARISHA BIASHARA

TANZANIA
Wadau wa sekta ya usafirishaji wamempongeza Mhe  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuimarisha biashara nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dakimp International Ltd, Ally Said Sleyyum amesema kuwa mazingira ya biashara yameboreshwa na hivyo kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi.
"Kwa muda mrefu, nimekuwa katika shughuli za biashara, haswa katika sekta ya uchukuzi, nimeona mabadiliko makubwa," amesema Bw Sleyyum.
Amesema kuzinduliwa kwa treni ya umeme ya Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kutasaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la wafanyabiashara kutoka nchi za Maziwa Makuu.
"Wateja wetu kutoka Mataifa ya Maziwa Makuu sasa watapata fursa ya kutumia muda mfupi katika usafirishaji wa bidhaa zao kwa kutumia SGR," amesema Bw Sleyyum ambaye kampuni yake imekuwa ikitoa na kusafirisha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha, amesema kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa mbalimbali nchini utasaidia pia katika ukuaji wa uchumi.
Kulingana naye, katika kipindi kifupi kijacho, Tanzania itakuwa kinara wa biashara katika ukanda wa maziwa makuu.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amebainisha kuwa, mazingira wezeshi yaliyowekwa na serikali yamefungua milango zaidi ya kibiashara, hasa katika kuondoa urasimu na ubabe kwa watendaji wa kodi.
"Zamani hali ilikuwa tofauti, mnadaiwa kodi kwa vitisho, leo hakuna mambo hayo, TRA na sisi walipakodi tunajadiliana na kulipa kodi bila vitisho," amefafanua.

"Kwa sasa hatuna mgogoro na TRA, tunashirikiana nao vizuri, mamlaka imejirekebisha sana," Ameongeza.