TAMASHA LA KIZIMKAZI LAFIKIA TAMATI, DKT SAMIA ANENA
ZANZIBAR
Tamasha la kizimkazi (Kizimkazi Festival) limefikia tamati leo Agosti 25, 2024 huku wageni kutoka maeneo mbalimbali wakihudhuria ,wakiongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Mwehe Kusini Unguja, visiwani Zanzibar.
Akizungumza kwenye kilele cha Tamasha hilo Mhe.Rais Dkt Samia amesema “Tamasha la kizimkazi lina lengo kubwa la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii,kuwaleta watu pamoja na kudumisha mila na desturi”.
Mhe Rais Dkt Samia ameshiriki kwenye matukio mbalimbali yaliyofanyika mwaka huu pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo rais wa benk ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi A. Adesina pamoja na ujumbe wake.
Aidha Tamasha la kizimkazi mwaka huu lilizinduliwa Agosti 18 huku likiwa na matukio mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa miradi, kuweka mawe ya msingi ya miradi, mafunzo ya shughuli za kiuchumi kwa vijana,michezo na maonesho ya tamadanuni.