MRADI WA MAJI MWANGA-SAME-KOROGWE MAMBO SAFI
Huu ni Mradi wa maji Mwanga-Same-Korogwe uliopo Mkoani Kilimanjaro uliokuwa umekwama kwa Miaka 10 sasa serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA), Mfuko wa Maendeleo wa Nchi Zinazozalisha Mafuta (OFID) na Kuwait Fund inaendelea kutekeleza na umefikia katika hatua ya nwishoni kukamilika.
Mradi huu utakapokamilika utasambaza maji katika Miji ya Same na Mwanga pamoja na vijiji 38 kwenye Wilaya za Same na Mwanga na vijiji vitano katika Wilaya ya Korogwe.
