MAAFISA UGANI MIFUGO & UVUVI WAPEWA PIKIPIKI 2762
DODOMA
Katika kipindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan jumla ya pikipiki 2762 zimetolewa kwa maafisa ugani wa mifugo na uvuvi ambazo zimetolewa katika awamu mbili ya kwanza Pikipiki 1562 na baadae 1200.
Pamoja na utolewaji wa pikipiki serikali imeiwezesha wizara ya mifugo na uvuvi kufanya zoezi la mafunzo rejea ya teknolojia na maarifa mbalimbali ya kisasa kwa maafisa ugani wa mifugo na uvuvi 3600 kati yao 3100 wa mifugo na wanaobaki wa uvuvi.
Aidha katika mwaka huu wa fedha Serikali imeridhia wizara hiyo kurejesha chanjo za mifugo ambapo Chanjo ya kuku itatolewa bure hususan kwa wafugaji wanawake nchini kote.