KAYA 951 KUUNGANISHWA NA GESI ASILIA
LINDI
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limezindua mpango wa kuunganisha kaya 951 na gesi asilia mwaka huu wa fedha.
Mradi huo utaunganisha kaya 451 za Lindi na kaya nyingine 500 za Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ili kupata chanzo hicho cha nishati safì na mpango huo ukikamilika utaongeza idadi ya kaya zilizounganishwa na matumizi ya gesi asilia 2451 nchi nzima.
Hivi sasa, kaya 891 za Dar es Salaam, 209 za Lindi na 400 za Mtwara zimeunganishwa kwenye mfumo wa usambazaji wa bomba la gesi asilia.
Mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia (2024-2034) unalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.