DKT SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUTUMIA BUSARA
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kushughulikia majukumu yao kwa weledi, kutumia busara na kufanya maamuzi sahihi pale inapobidi.
Katika hotuba yake aliyoitoa Agosti 15, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya hafla ya kuwaapishwa viongozi wateule ameeleza kuwa mabadiliko ya hivi karibuni ni sehemu ya juhudi za kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali.
“Umekula viapo viwili, kimoja kwa Mungu wako, kwa imani yako, na kwa Watanzania na kingine ni kiapo cha uadilifu.
Hata hivyo, nitakutana na kila mmoja wenu binafsi katika sekta zenu kwa majadiliano zaidi,” Rais Samia amesema.