BARABARA KM 13,035.64 ZATENGENEZWA
TANZANIA
Serikali imefanya matengenezo ya kawaida ya barabara za mijini na vijijini zenye jumla ya urefu wa wa kilomita 13,035.64.
Mgawanyo wa barabara hizo ni pamoja na matengenezo ya kawaida ya barabara zenye urefu wa kilomita 9,838.80, matengenezo ya barabara za lami zenye urefu wa kilomita 115.97 na matengenezo ya barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 3,080.87
Vilevile serikali imefanya ukarabati wa madaraja na makalavati 17 na mifereji ya kuondoa maji barabarani mita 51,309.62 katika maeneo mbalimbali nchini.