VIONGOZI WAAPISHWA, DKT SAMIA AWAONYA

 

VIONGOZI WAAPISHWA, DKT SAMIA AWAONYA

VIONGOZI WAAPISHWA, DKT SAMIA AWAONYA

DAR ES SALAAM
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Julai 26 amewaapisha viongozi mbalimbali, Ikulu jijini Dar es salam  aliowateua siku za hivi karibuni.
Akizungumza katika hafla ya uapisho huo Mhe Rais Dkt  Samia amewataka viongozi hao kuongoza kwa kuzingatia katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwatumikia wananchi “Niombe sana nendeni katumikieni wananchi, sitarajii muende mkawadhihaki”amesema
Aidha Dkt Samia amesisitiza viongozi kutanguliza maslahi ya wananchi mbele “hakikisheni maslahi ya wananchi yanapatikana,kiapo kinapiga,ukikiendea upande hakitakuacha kitakupiga” amesema Dkt Samia.
Vile vile amewapa onyo viongozi wanaotumia madaraka kwa kujinufaisha wao wenyewe  “wale mliozoea kutumia nafasi zenu kujinufaisha au kujinyanyua nyinyi  kabla ya kunyanyua taifa, kama upo kwenye madaraka rekebisha kabla sijakuona,kama ndio unaingia tambua hilo”Ameongeza.