TSH BIL 6.3 ZAWAPA MINARA 47 WAKAZI 866,352 WA KIGOMA
KIGOMA
Kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kimewanufaisha wakazi wapatao 866,352 kupitia huduma bora za mawasiliano katika Mkoa wa Kigoma, kutokana na mradi wa minara ya simu 47 iliyojengwa na kuanza kutumika mkoani humo.
Wilaya zilizofaidika na minara hiyo na idadi ya minara iliyojengwa, kwenye mabano ni Buhigwe (6), Kakonko (12), Kasulu DC (6), Mji wa Kasulu (5), Kibondo (8), Kigoma DC (2) na Uvinza (8).
Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa 26 Tanzania Bara, itakayonufaika na mradi wa minara 758 inayoendelea kujengwa nchi nzima na inayotarajiwa kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 8.5 itakapokamilika mwanzoni mwa mwaka 2025.
