“VIONGOZI TUISHI KWENYE MISINGI YA UONGOZI BORA” DKT SAMIA
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kujijengea utamaduni wa kuishi kwenye misingi ya uongozi bora kwa kuwa waadilifu,na wenye kusema yanyosadikika.
Dkt Samia ametoa wito huo leo juli 5 wakati akihutubia kwenye kongamno la wanawake wa kiislam lililofanyika katika hotel ya golden Tulip Zanzibar.
“Sisi viongozi tunao wajibu wa kuishi katika misingi ya uongozi bora,tunatakiwa kuwa waadilifu, ukilisema liwe ndilo,sio leo umesema hili, kesho watu wakikuuliza umesema lile”Amesema Rais Samia
Pia Mhe Rais Samia amesema viongozi wanapaswa kuwa weledi “unapokuwa kiongozi, uwe mweledi, wanapokuja watu na shida zao unasikiliza halafu unajua njia za kuwapitisha na kupata utatuzi wa shida yao” Ameongeza Dkt Samia.