MBINGA YAPEWA TSH BIL 11.97

 

MBINGA YAPEWA TSH BIL 11.97

MBINGA YAPEWA TSH BIL 11.97 

RUVUMA
Ndani ya kipindi cha miaka mitatu zaidi ya Shilingi bilioni 11.97 zimetumika wilayani Mbinga katika utekelezaji wa miradi ya sekta za elimu, afya, maendeleo ya jamii, kilimo, utawala, biashara na mifugo.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo, mwaka 2021/22, Halmashauri hiyo ilipokea shilingi bilioni 5.6, mwaka 2022/23 bilioni 5.4 na hadi Disemba 2023 jumla ya milioni 974.6.