TANZANIA, KONGO DRC KUSHIRIKIANA MAENEO YA BANDARI
DRC
Serikali za Tanzania na Congo (DRC) zimesaini Mkataba wa pamoja wa Ushirikiano katika uendelezaji na Uendeshaji wa bandari kavu ambazo zitajengwa katika maeneo maalum ya Kwala - Pwani na Katosho-Kigoma kwa Tanzania na Kasambondo - Jimbo la Kalemie Tanganyika DRC; Kasumbalesa na - Jimbo la Haut Katanga DRC.
Mkataba huo umetiwa saini jijini Lumbumbashi Nchini DRC Juni 2024 ambapo kwa niaba ya Serikali ya JMT umewakilishwa na Naibu Waziri Wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na upande wa Serikali ya JKC uliwakilishwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Marc Ekila Likombo.
Kwa Serikali ya Tanzania itatenga hekta 15 za ardhi katika eneo la Katosho- Kigoma na Hekta 45 katika eneo la Kwala- Pwani sambamba na kutoa Hati Miliki kwa ajili ya DRC kujenga na kuendesha Bandari Kavu huku Upande Congo -DRC Serikali itatenga Hekta 15 katika eneo la Kasumbalesa na Hekta 20 katika eneo la Kasenga-Jimbo la Haut Katanga na Hekta 25 katika eneo la Kasambondo- Kalemie Jimbo la Tanganyika sambambana kutoa Hati Miliki kwa ajili ya Serikali ya Tanzania kujenga na kuendesha bandari Kavu.
Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha usafirishaji na uchukuzi unarahisishwa hususani kwa mzigo mkubwa unaosafirishwa na DRC kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
ZINGATIA:- Mkataba huo unatarajiwa kuongeza ufanisi na idadi ya mizigo inayosafirishwa katika mnyororo mzima wa Uchukuzi ambapo kwa sasa takwimu zinazonesha kwa 2022/23 tani Mil. 3.5 za mzigo wa Kongo zilihudumiwa kupitia Bandari ya Dar.