TSH MIL 742+ ZIMEWAPA SHULE KITUMBALOMO

 

TSH MIL 742+ ZIMEWAPA SHULE KITUMBALOMO

TSH MIL 742+ ZIMEWAPA SHULE KITUMBALOMO

RUVUMA 
Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imetoa kiasi cha shilingi 742,509,99.8 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kitumbalomo iliyopo Kata Kitumbalomo Kijiji cha Liwihi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambayo ujenzi wake umeshakamilika na shule hiyo imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza januari 2024.
Pamoja na shule hiyo mpya pia Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea tena fedha shilingi 560,552,827 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQIP fedha ambayo itakwenda kutekeleza ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Muungano.
Aidha katika kuboresha mazingira rafiki kwa walimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea kiasi cha shilingi 95,000,000 kwa ajili ya kujenga nyumba ya walimu( two in one) katika shule ya Sekondari Kitumbalomo. 
Hizi ni jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Elimu nchini.