TSH MIL 190 KUKARABATI MIUNDO MBINU KISHAPU
SHINYANGA
Serikali imepeleka shilingi 190,000,000.00 kwa TARURA Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuanza kufanya matengenezo ya dharura kwa baaadhi ya maeneo ya barabara ziizoharibiwa na mvua.
Serikali imefanya tathimini ya mtandao mzima wa barabara katika Wilaya ya Kishapu na kubaini ukubwa wa uharibifu ambapo shilingi 2,553,415,000.00 zinahitajika ili kuzifanyia matengenezo barabara hizo.