TSH BIL 66.7 KUNUNUA VIFAA TIBA
TANZANIA
Serikali imetenga shilingi bilioni 66.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika mwaka 2024/25, ikiwemo mashine za X-ray, (kwa mujibu wa TAMISEMI).
Kwa kuonesha utekelezaji wa lengo hilo kwa vitendo, serikali imekuwa ikipandisha bajeti ya Wizara ya Afya kila mwaka ili kuunga mkono azma hiyo ambapo katika kipindi cha miaka ya fedha 2021/22 hadi 2023/24, Serikali ilinunua na kufunga jumla ya mashine 280 za kidigitali za X-ray na mashine 322 za Ultra sound katika vituo vya afya vya msingi.
