TSH BIL 56.038 ZAJENGA KM 39

 

TSH BIL 56.038 ZAJENGA KM 39

TSH BIL 56.038 ZAJENGA KM 39 

MWANZA
Katika kipindi cha mwaka 2023/2024 serikali imetekeleza miradi 7 ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mkoa wa Mwanza yenye urefu wa kilomita 39 ambapo gharama za miradi hiyo ni Shilingi Bilioni 56.038.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Ujenzi wa kilomita 10 za kiwango cha lami katika barabara ya Isandula (Magu)- Hungumalwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 14.099, Ujenzi wa kilomita 3.0 za barabara ya Mabuki- Jojiro- Ngudu yenye gharama ya shilingi Bilioni 3.495.
Aidha jumla ya shilingi bilioni 18.406 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya Ujenzi wa kilomita 10.0 za barabara ya Mwanza Airport - Kayenze - Nyanguge kwa kiwango cha lami,Ujenzi wa kilomita 3.0 za barabara ya Bukokwa - Nyakalilo kwa kiwango cha lami  ambao utatumia Shilingi Bilioni 3.402.
Pia serikali imetenga Shilingi Bilioni 9.206 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 7.0 kwa kiwango cha lami kuanzia Nansio mpaka Rugezi 
Vilevile serikali kupitia TANROADS inatarajia kutumia shilingi Bilioni 3.898 kwa ajili ya Ujenzi wa kilomita 3.0 kwa kiwango cha lami kwenye barabara ya Mwanangwa - Misasi- Salawe- Kahama 
Hali kadhalika serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 3.529 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kamanga - katunguru- sengerema kwa kiwango cha lami ambapo kwa sasa Mkandarasi anaendelea na kazi za ujenzi wa makalavati, maboksi kalavati pamoja na matabaka ya chini ya barabara (G7 & G15).