DKT SAMIA AMPONGEZA SIR KEIR STARMER
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametuma salam za pongezi kwa kwa Sir Keir Starmer kwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa chama cha labour cha uingereza na kuwa waziri mkuu wa uingereza.
Kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii X na Instagram Mhe Dkt Samia ameandika
“On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to Sir Keir Starmer on the UK Labour Party electoral victory and on becoming the Prime Minister of the United Kingdom. I look forward to continued cooperation and partnership between Tanzania and the United Kingdom in addressing global challenges and fostering economic development for the people of our two countries”.
(Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Sir Keir Starmer kwa ushindi wa uchaguzi wa Chama cha Labour cha Uingereza na kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
Natarajia kuendelea kwa ushirikiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza katika kutatua changamoto za kimataifa na kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa watu wa nchi zetu mbili.)
BimkubwaTanzania tunaungana na Rais wetu kukupongeza na kukutakia majukumu mema.