TSH BIL 400 KUTEKELEZA RLGSP
DODOMA
Kiasi cha shilingi bilioni 400 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya Uimairishaji wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Regional and Local Government Strengthing Programme- RLGSP) ambao utakamilika mwaka 2030 huku wastani wa Shilingi bilioni 16 zikiwa zimetumika tangu kuanza kwake mwaka 2021.
Malengo maalum ya programu hii ni kukuza maendeleo ya kiuchumi ndani ya mikoa na mamlaka za serikali za mitaa, lakini pia kuboresha utoaji wa huduma kupitia usimamizi bora wa kifedha, utawala na rasilimali watu.
Aidha utekelezaji wa RLGSP utaongozwa na malengo na mikakati inayolenga kwa pamoja kutekeleza azma ya kina ya kugatua na kupanua huduma za umma na hali za kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.