TSH BIL 434.9 KUZIMA JENERETA NA KUWASHA GRIDI YA TAIFA
KIGOMA
Kiasi cha shilingi bilioni 434.9 kimetumika Mkoani Kigoma kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kituo kidogo cha kupokea umeme wa msongo wa kilovolt 220 eneo la Kidahwe, ili kuwezesha umeme wa gridi kuanza kutumika kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kuachana na matumizi ya mashine za mafuta (jenereta) ifikapo Septemba 30 mwaka huu.
Pamoja na zoezi la ujenzi wa kituo kidogo cha kupokea umeme mradi huo pia unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovolt 400 kutoka Nyakanazi Kwenda kituo cha kupokea umeme kinachojengwa Kidahwe nje kidogo ya mji wa Kigoma na ujenzi wa kituo kikubwa cha kupokea umeme wa msongo wa Kilovolt 400.