SOKO LA KARIAKOO KUFUNGULIWA AGOSTI 2024

 

SOKO LA KARIAKOO KUFUNGULIWA AGOSTI 2024

SOKO LA KARIAKOO KUFUNGULIWA AGOSTI 2024

DAR ES SALAAM
Wafanyabiashara wataanza tena biashara katika soko la kariakoo lililokarabatiwa kuanzia mwezi ujao, baada ya soko la awali kuungua kwa moto Julai 10, 2021 na serikali kutoa shilingi bilioni 28 kwa ajili ya ujenzi  wa soko jipya lenye ghorofa 8.
Mkurugenzi wa masoko ya kariakoo Bi  Hawa Ghasia amesema bodi imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo, hivyo kuashiria kuwa masoko yatakuwa tayari kutumika ifikapo mwezi Agosti.
"Tumekagua maeneo, na kwa ujumla tumefurahishwa na kasi ya ujenzi, ingawa tunamtaka mkandarasi kuharakisha kazi kwa sababu tuna mpango wa kuwahamisha wafanyabiashara katika masoko haya ifikapo Agosti," alisisitiza  Bi Ghasia.
Kwa mujibu wa Ghasia, zaidi ya wafanyabiashara 800 ambao awali walikuwa na vibanda katika masoko hayo wametambuliwa na watatengewa maeneo ndani ya masoko hayo mawili.
Orodha ya wafanyabiashara hao itapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi), tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, katika ofisi ya Meneja wa Soko la Kisutu, na ile ya meneja wa Machinga Complex.
Wafanyabiashara wapya watakuwa na mchakato wa uwazi wa kuomba kujiunga na masoko kupitia Tovuti ya Tausi.
KUMBUKA:- Masoko yote mawili yameimarishwa kwa mifumo maalum ya kuzima moto iliyowekwa katika kila duka na sura ya biashara ili kuzuia ajali za moto za baadaye.