TSH BIL 42 KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI IFAKARA
MOROGORO
Kiasi cha shilingi bilioni 42 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya maji kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kiburubutu ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba na utakapokamilika unatarajiwa kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Mji wa Ifakara.
