TSH BIL 82.635 ZABORESHA MIUNDOMBINU NJOMBE
NJOMBE
Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 82.635 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Isyonje – Kikondo – Makete Km 96.2 (Sehemu ya Kitulo – Iniho Km 36.3) na Ujenzi wa Mzani wa Igagala ambapo kazi zote hizo zipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji ambapo ujenzi wake utakamilika Julai 11, 2026.
