TSH BIL 2.6 ZAWAINUA WANANCHI WA MBINGU NA IGIMA
MOROGORO
Katika kuendeleza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani, serikali ya awamu ya sita imepeleka kiasi cha shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji katika kata za Mbingu na Igima zilizopo katika Halmshauri ya wilaya Mlimba Mkoani Morogoro.
Utekelezji wa mradi huo umefikia 85% na unatarajiwa kukamilika mwaka huu (2024) na utakapokamilika utawanufaisha wananchi wanaoishi katika vijiji saba vinavyopatikana ndani ya kata ya mbingu na igima.