DAR KUWA KITOVU CHA TEKNOLOJIA AFRIKA
NIGERIA
Tovuti ya Business Insider Afrika yenye makao yake makuu Ikeja, Lagos nchini Nigeria imeutaja Dar es salaam iliyopo nchini Tanzania kuwa ni miongoni mwa miji 10 inayotarajiwa kuwa kitovu cha teknolojia kwa mwaka mmoja ujao barani Afrika.
Miji hiyo ni
1. Victoria, Ushelisheli/ Seychelles
2. Addis Ababa, Ethiopia
3. Luanda, Angola
4. Dar es Salaam, Tanzania
5. Algiers, Algeria
6. Bamako, Mali
7. Lusaka, Zambia
8. Harare, Zimbabwe
9. Mogadishu, Somalia
10.Abidjan,Ivory Coast
Kwa mujibu wa business Insider Afrika inasema hatua hii inachagizwa na taarifa kutoka kwenye ripoti kutoka kwa STARTUP BLINK inayoitwa Ripoti ya Mfumo wa Mazingira ya Kuanzisha 2024, ambayo inaangazia mifumo bora ya kiteknolojia kwenye dunia.
Ripoti hiyo pia imeorodhesha baadhi ya vituo vya teknolojia vinavyoibukia duniani ambavyo inavitaja kama Startup Blink titled Startup Ecosystem Report 2024, "Mifumo ya Mazingira ya Washindani."