KAMPUNI 27 UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA

 

KAMPUNI 27 UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA

KAMPUNI 27 UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA

DAR ES SALAAM
UJumbe wa wafanyabiashara kutoka kampuni 27 za Ufaransa ulikuja nchini Siku za hivi karibuni kwa ajili ya kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji.
Wafanyabiashara hao wamejadili namna ya kuwekeza Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo, teknolojia za miundombinu, nishati, usafirishaji na Maendeleo ya miji.
Pamoja na uwekezaji katika sekta hizo,pia ziko fursa kubwa za masoko nchini Ufaransa kwa bidhaa za kahawa,samaki na hata mbegu za mbogamboga .
Kwa mujibu wa takwimu za Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ufaransa imewekeza Tanzania katika miradi 41 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 104.34 ambayo imetoa ajira 2379 katika maeneo ya kilimo, ujenzi, usafirishaji, huduma,taasisi za fedha pamoja na rasilimali watu.