SETI, VICHWA VYA TRENI VYATUA NCHINI
DAR ES SALAAM
Serikali kupitia shirika la Reli Tanzania (TRC) imepokea Seti mbili za treni ya kisasa ya umeme (Electric Multiple Unit-EMU) na vichwa nane vya treni nchini toka Korea ya Kusini na kutimiza jumla ya seti 3 zilizowasili nchini mpaka sasa (seti ya kwanza iliwasili mwezi April 2024 ambayo inaendelea na majaribio.
Serikali kupitia TRC ilifanya manunuzi ya seti 10 za treni ya EMU zinazotengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea Kusini ambapo seti moja ya EMU ina jumla ya mabehewa nane yakijumuisha kichwa kimoja mbele na kingine nyuma ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 589 na kutembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa
Aidha hadi sasa shirika la reli Tanzania limeshapokea jumla ya mabehewa 65 ya abiria, vichwa 17 vya umeme na seti tatu za EMU.
Kadhalika TRC inajiandaa kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni za umeme kupitia reli ya kiwango cha kimataifa kati ya Dar es salaam mpaka Dodoma kuanzia Julai 25, 2024.
