SAMIA HOUSING SCHEME, KAWE, KUKAMILIKA 2024
DAR ES SALAAM
Mradi wa Samia Housing Scheme,unaojengwa katika eneo la Kawe, Ukwamani jijini Dar Es Salaam ujenzi Umefikia katika ghorofa ya 10, (ya mwisho kwa sababu unahusisha ghorofa 10) ambao utaziweka pamoja kaya zipatazo 560 katika eneo hilo na kinachoendelea hivi sasa ni kufunga mfumo wa umeme, kupiga plasta ghorofa zote kujenga uzio na kufanya umaliziaji.
Mradi wa SAMIA HOUSING SCHEME, wa Kawe Dsm ulianza mwishoni mwa mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika mwishoni 2024, huku ukihusisha idadi ya Nyumba 5,000, kwa gharama ya shilingi bilioni 260, Kati ya nyumba hizo, 50% zitajengwa Dsm, 20% zitajengwa Dodoma na 30% kwingineko nchini.
