TANZANIA ,MSUMBIJI KUFUNGUA KITUO CHA FORODHA MTAMBASWALA

 

TANZANIA ,MSUMBIJI KUFUNGUA KITUOC HA FORODHA MTAMBASWALA

TANZANIA ,MSUMBIJI KUFUNGUA KITUO CHA FORODHA MTAMBASWALA

DAR ES SALAAM
Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kufungua kituo kimoja cha forodha katika eneo la Mtambaswala wilayani Masasi Mkoani Mtwara  kitakachohamasisha biashara kati ya nchi hizo mbili ili kuongeza kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Msumbiji ambapo mwaka 2022  thamani ya biashara kati ya nchi hizo ilikuwa takribani dola milioni 57.8.
Kauli ya makubaliano hayo imetolewa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  Ikulu Jijini Dar es salaam akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe Filipe Nyusi wakati wakizungumza na vyombo vya habari baada ya mapokezi ya Rais wa Msumbiji aliyekuja nchini kwa ziara ya Kiserikali kuanzia Julai Mosi hadi 4, 2024.
Pamoja na kuanzishwa kwa kituo cha Forodha Mhe Rais Dkt Samia amesema Ma-Rais hao wamekubaliana pia Kuongeza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji.