CCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA USIMAMIZI WA ILANI

 

CCM  YAMPONGEZA RAIS SAMIA USIMAMIZI WA ILANI

CCM  YAMPONGEZA RAIS SAMIA USIMAMIZI WA ILANI

MTWARA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amempongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vyema Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 nchini kote ikiwemo Mkoa wa Mtwara.
Dkt Nchimbi amesema Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 mkoani Mtwara imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 80.
"Mkuu wa Mkoa ametoa taarifa ya maendeleo ya miradi yote mkoani humu, utekelezaji wa Ilani ya Chama unazidi asilimia 80," Dk Nchimbi amesema  hayo  Julai 28, 2024 wakati wa mkutano wa hadhara Mtwara Mjini uliofanyika kwenye Uwanja wa Saba Saba.
Ameongeza "tunamshukuru Rais wetu kwa kusimamia ilani ya chama kwa ufanisi nchini kote,"
Aidha, Dkt Nchimbi amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kushirikiana na serikali kwa ajili ya utekelezaji kamili wa ilani.