“MIFUMO ISOMANE KABLA YA DISEMBA 2024” DKT SAMIA

 

“MIFUMO ISOMANE KABLA YA DISEMBA 2024” DKT SAMIA

“MIFUMO ISOMANE KABLA YA DISEMBA 2024” DKT SAMIA

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya  habari , mawasiliano na teknolojia ya habari kuhakikisha mifumo ya serikali inayosaidia kutoa huduma inasomana kabla ya mwezi Disemba 2024.
Mhe Rais  Samia ametoa  agizo hilo Leo Julai 29 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) lililofanyika Ikulu Dar es Salaam.
Amesema “Nitumie jukwaa hili kuikumbusha wizara kuhakikisha kwamba lile agizo langu la mifumo kusomana  ifikapo Disemba 2024 liendelee kufanyiwa kazi”.
Aidha Mhe Rais Samia amesisitiza wizara hiyo kuendelea kufanya ufuatiliaji wa kuhakikisha mifumo yote mipya inayotenegenezwa nayo inasomana na mifumo iliyopo.
Dkt Samia amesisistiza “ Mifumo yetu ikisomana inapunguza gharama zisizo za lazima, lakini pia inapunguza uzembe na kuziba mianya ya Rushwa.