WASAFIRI 8,375,047 WALIPIMWA EBOLA, MARBURG NK
TANZANIA
Serikali kupitia Wizara ya afya imeendelea kudhibiti kuingia kwa magonjwa hatari yanayoambukiza ikiwemo Ebola, Marburg, mafua ya Ndege (SARS), UVIKO-19, Homa ya manjano, pamoja na Homa ya Nyani (M-Pox) kuingia kupitia maeneo ya viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu kwa kufanya uchunguzi wa afya kwa wasafiri wanaotoka katika nchi mbalimbali kuangalia endapo wana magonjwa hatari ya kuambukiza.
Katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, jumla ya wasafiri 8,375,047 walikaguliwa ambapo 1,733,502 sawa na 20.7% ni wasafiri wa nje (International Travelers) na wa ndani (domestic) ni 6,641,545 sawa na 79.3% ambapo hakuna msafiri aliyegundulika kuwa na magonjwa hatari ya kuambukiza.
Aidha katika kudhibiti ugonjwa wa Homa ya Manjano, wasafiri 5,642,611 walikaguliwa kama wamepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano ambapo wasafiri 11,747 walichanjwa chanjo ya ugonjwa huo, ikilinganishwa na wasafiri 4,889,591 waliokaguliwa na 10,583 waliochanjwa kipindi kama hiki mwaka 2022/23.