BIASHARA TANZANIA NA INDIA YAFIKIA TRIL 20+
DAR ES SALAAM
Biashara baina ya Tanzania na India imepanda hadi dola za Marekani bilioni 7.9 ( shilingi 20,145,000,000,000) katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, na kuashiria ukuaji wa 22% ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Ukuaji huu umeipandisha Tanzania kwenye nafasi ya mshirika wa pili wa biashara wa India kwa ukubwa barani Afrika.
Takwimu za hivi punde za biashara zinaonesha sio tu ongezeko la kiasi cha biashara baina ya nchi hizo mbili bali pia kuboreka kwa usawa wa kibiashara.
Kwa mujibu wa takwimu za TRA kwa mwaka wa 2023, India inaongoza kwa kuwa soko la nje la Tanzania, na mauzo ya nje kwenda India yakipita yale ya soko kubwa zaidi la Tanzania kwa zaidi ya 50%.
Katika mwaka uliopita pekee, wajumbe na wafanyabiashara wa India walitembelea Tanzania, na kuchangia katika kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Uwekezaji wa India nchini Tanzania unahusisha sekta za hospitali, dawa, chanjo za wanyama, elimu, madini, na usindikaji wa mazao ya kilimo.