WANANCHI URU KUSINI KUJENGEWA KITUO CHA AFYA

 

WANANCHI URU KUSINI KUJENGEWA KITUO CHA AFYA

WANANCHI URU KUSINI KUJENGEWA KITUO CHA AFYA

KILIMANJARO
Serikali imepanga kujenga kituo cha afya katika kata Uru Kusini  iliyopo katika wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, hatua ambayo itasaidia kumaliza kero ya wananchi wa kata hiyo na maeneo jirani  waliokuwa wanapata adha ya  kufuata huduma hizo umbali mrefu.
Aidha pamoja na mpango huo serikali kupitia bajeti ya fedha ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Afya, wametenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba na vitasambazwa katika vituo vyote vya afya nchini. 
Hatua ya utekelezaji huo ni maelekezo ya  Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anataka kuona nchini kote kunakuwa na vifaa tiba vya kisasa vinavyopatikana katika ngazi ya zahanati na ngazi ya vituo vya afya.