TSH BIL 84 KUJENGA BARABARA MVUGWE- NDUTA KM 59.35
KIGOMA
Kiasi cha shilingi bilioni 84 kutoka kwa serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kinajenga barabara ya Mvugwe - Nduta (Km 59.35) Mkoani Kigoma ambapo kwa sasa mradi umetekelezwa kwa 81.49% na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2024.
Aidha ujenzi wa mradi huo umehusisha pia na Ujenzi wa daraja la Malagarasi lenye urefu wa mita 77 na madaraja mengine mawili ambayo yote yamekamilika kwa 100%.
ZINGATIA:- Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuufungua Mkoa wa Kigoma kupitia Miundombinu ya barabara na hivyo kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kati ya Mkoa huo na Mikoa jirani ya Geita, Mwanza pamoja na nchi jirani za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
