WANACHAMA 4,230,368 WAJIUNGA NA iCHF
TANZANIA
Mwaka 2022/23, idadi ya wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa - iCHF iliongezeka kwa 9.0% na kufikia wanachama 4,230,368 (kaya 872,013) kutoka wanachama 3,862,266 (kaya 863,195) mwaka 2021/22.
Ongezeko hilo limetokana na elimu iliyoendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na umuhimu wa kujiunga na Mfuko.
Katika kipindi hicho, jumla ya vituo 6,755 vilitoa huduma kwa wanachama wa Mfuko ikilinganishwa na vituo 6,378 mwaka 2021/22.
Kati ya hivyo, vituo vya umma vilikuwa 6,733, vituo vya taasisi za kidini vilikuwa 20 (vituo vya afya vitatu na zahanati 17), na zahanati mbili za watu binafsi.
Vituo vinavyomilikuwa na Serikali vilijumuisha zahanati 5,723, vituo vya afya 807, hospitali za Halmashauri 175, na hospitali za rufaa za mikoa 28.