TSH MIL 800+ KUWAONGEZEA MAJI KIBAHA

 

TSH MIL 800+ KUWAONGEZEA MAJI KIBAHA

TSH MIL 800+ KUWAONGEZEA MAJI KIBAHA

PWANI
Jumla ya wakazi wapatao 1,872 wa Vitongoji vya Miyombo Ufugaji, Ukulima na Mizunguni 'B' katika Kijiji cha Lukenge na sehemu ya Kijiji cha Mizuguni Kata ya Magindu wilayani Kibaa Mkoani Pwani  wako mbioni kuongezewa wigo wa upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao.
Hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu , mradi wa maji Miyombo unaogharimu Shilingi 802,529,650 ambao unasimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Wilaya ya Kibaha kutoka chanzo cha maji cha kisima kirefu utakuwa umekamilika.
Hadi hivi sasa mradi umefikia 45%  tangu ulipoanza  kutekelezwa Oktoba 2023 na kazi zilizofanyika mpaka sasa ni pamoja na ujenzi wa mhimili wa tanki wenye mita 12, ujenzi wa kitako cha tenki la lita 50,000 unaendelea pamoja na  kazi nyingine zinaendelea ili kukamilisha kwa muda mradi huo.
Mradi huo utakapokamilika utaongeza huduma ya maji kwa 1% kwa wananchi waishio Vijijini kwa Wilaya ya Kibaha na kufikisha 79% kutoka 78% iliyopo sasa huku lengo likiwa ni kufikia 85% ifikapo Desemba 2025.