MELI KUBWA YA MIZIGO YATIA NANGA BANDARINI DAR

 

MELI KUBWA YA MIZIGO YATIA NANGA  BANDARINI DAR

MELI KUBWA YA MIZIGO YATIA NANGA  BANDARINI DAR

DAR ES SALAAM
Bandari ya Dar es Salaam juni 22 imepokea meli kubwa zaidi ya mizigo kuwahi kuwa na urefu wa mita 294.12 na kubeba makontena 4,000, kutokana na upanuzi mkubwa wa bandari hiyo na kuimarika kwa ufanisi.
Meli hiyo ilitia nanga katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na jumla ya makontena 4000 ambapo meli hiyo ina uwezo wa kubeba hadi kontena 4,700.
Hatua hii imefikiwa kutokana na uboreshaji wa miundombinu iliyohusisha uchimbaji wa kina cha bandari, upanuzi wa njia ya kuingilia kwenye gati, ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya kisasa vya kutunzia mizigo kumesababisha kuwasili kwa meli kubwa ya kwanza ya makontena jijini Dar es Salaam inayotarajiwa kufungua milango kwa makampuni mengine kutumia kituo cha baharini.
Itachukua siku tano  tu kwa shehena yote iliyobebwa kwenye meli hiyo kupakuliwa, ikiwa ni pamoja na kupakia makontena kabla ya kuondoka.