VIJIJINI WATAPATA MAJI SAFI KWA 85% MWAKA 2025

 

VIJIJINI WATAPATA MAJI SAFI KWA 85% MWAKA 2025

VIJIJINI WATAPATA MAJI SAFI KWA 85% MWAKA 2025

TANZANIA
Serikali ina azma ya kuhakikisha wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanapata huduma bora na endelevu ya maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025. 
Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imeendelea na jitihada za kujenga na kukarabati miradi ya maji pamoja na kupanua mitandao ya kusambaza maji na kuimarisha usimamizi wa huduma ya maji vijijini. 
Jitihada hizo zimewezesha kuongezeka kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kutoka wastani wa 77% mwezi Desemba, 2022 hadi kufikia wastani wa 79.6% mwezi Desemba, 2023. 
Kiwango kilichoongezeka kimetokana na kutekelezwa kwa miradi 632 yenye vituo vya kuchotea 7,956 vyenye uwezo wa kuhudumia wananchi 4,740,959. 
Aidha hali hiyo, inafanya jumla ya wananchi wa vijijini wanaopata huduma ya maji kufikia 34,950,368 kati ya wananchi 39,232,999 waishio vijijini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.