UJENZI BANDARI ZA KIBIRIZI NA UJIJI WAFIKIA 98.60%
KIGOMA
Mradi wa ujenzi wa Bandari za Kibirizi unaohusisha ujenzi wa gati, uongezaji wa kina, maghala ya mizigo, jengo la abiria na ofisi mbili (2) na bandari ya Ujiji unaohusisha ujenzi wa gati jengo la abiria, jengo la kuhifadhi mizigo, ujenzi wa uzio na kuongeza kina umefikia 98.60%.
KUMBUKA:- Serikali imeendelea kuongeza wigo wa huduma zake za kibandari kwa kujenga bandari katika maziwa makuu nchini ikiwemo za Ziwa Tanganyika.
