TSH MIL 580 ZAWAPA NAFUU WANAFUNZI RORYA
MARA
Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepeleka fedha shilingi Milioni 580 kupitia mradi wa SEQUIP na kujenga shule mpya ya Sekondari ya Ingri iliyopo katika wilaya ya Rorya Mkoani Mara.
Hapo awali wanafunzi wa Vijiji vya Malongo, Ingri na Ruanda walikuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya Km 22 kwa siku kufuata shule ya Sekondari sasa wamejengewa shule mpya karibu na makazi yao.
