USIMAMAMIZI MZURI WAIUZA KAHAWA SH ELFU 5+ @KG
KAGERA
Wakulima wa kahawa Mkoani Kagera wana kila sababu ya kutabasamu, hii ni kwa sababu kwa mara ya kwanza kilo moja ya kahawa imenunuliwa kwa zaidi ya shilingi 5,000 katika mnada uliofanyika Juni 18, mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa Meneja wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) Mkoa wa Kagera, Edmond Zani
Katika mnada uliofanyika Juni 18 mwaka huu, AMCOS ya Ruhoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba iliuza jumla ya kilo 71,369 za kahawa aina ya Robusta ambapo kilo moja iliuzwa kwa shilingi 5,233
AMCOS ya Kafunjo ya Karagwe iliuza jumla ya shilingi 93,378 ambapo kilo moja ilifikia 5,230 huku Kamahungu AMCOS ya Karagwe DC ikiuza jumla ya kilo 4,621 huku kilo ikiuzwa 5,310
Aidha taarifa kutoka wizara ya kilimo inasema Serikali inafanya kila iwezalo kutafuta wawekezaji watakaoweza kuanzisha kiwanda cha kusindika mazao kwa ajili ya kuongeza thamani ambacho kitasaidia wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao.