MUHIMBILI YAJIPANGA KUELEKEA AFCON 2027

 

MUHIMBILI YAJIPANGA  KUELEKEA  AFCON 2027

MUHIMBILI YAJIPANGA  KUELEKEA  AFCON 2027

DAR ES SALAAM
Wakati Tanzania ikijiandaa kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027,  kwa kushirikiana nan chi za Kenya na Uganda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imejipanga kikamilifu kutoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wachezaji watakaoshiriki fainali hizo zinazosubiriwa kwa hamu.Hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH (Upanga & Mloganzila), Profesa Mohamed Janabi.
Utoaji wa huduma bora unatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kutoa mafunzo kwa wataalam, ununuzi wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi ili kuboresha huduma za afya nchini.
KUMBUKA:- Tanzania, Kenya, na Uganda zilichaguliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 ambapo kwa Tanzania michezo hiyo inatarajiwa kuandaliwa jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, New Amaan Kiwanja cha Zanzibar na Uwanja mpya wa Samia Suluhu Hassan unaoendelea kujengwa mkoani Arusha.