HADI MWAKA 2025 MIJINI MAJI YATAPATIKANA KWA 95%

 

HADI MWAKA 2025 MIJINI MAJI YATAPATIKANA KWA 95%

HADI MWAKA 2025 MIJINI MAJI YATAPATIKANA KWA 95%

TANZANIA
Serikali kupitia Wizara ya maji  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miradi ya maji. 
Lengo ni kuhakikisha zaidi ya 95% ya wakazi wa mijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025. 
Hadi mwezi Desemba 2023, upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini umefikia wastani wa 90% ikilinganishwa na wastani wa 88% katika kipindi kama hicho mwaka 2022.
Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa miradi 85 ya maji inayohudumia wakazi 4,641,505 wa maeneo ya mijini.