MABORESHO MIUNDO MBINU BANDARI YA KWALA YAENDELEA
PWANI
Serikali inaendelea kufanya maboresho katika Bandari Kavu ya Kwala, miongoni mwa maboresho hayo ni pamoja na ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa kilomita 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro hadi Bandari Kavu ya Kwala ambao umekamilika na ujenzi wa yadi ya sakafu ngumu (pavement) yenye ukubwa wa hekta tano (5) kwa ajili ya kuhifadhi shehena unaendelea na utekelezaji wake 96%.
Bandari Kavu hiyo imeanza kutoa huduma za kibandari kwa kutoa makasha kutoka bandari ya Dar es salaam na kwenda Kwala kwa kutumia njia ya reli.
