BARABARA MALAGARASI-UVINZA KUKAMILIKA MACHI 2025
KIGOMA
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza (Km 51.1) kwa kiwango cha lami unaotekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Abu Dhabi na OPEC kwa gharama ya Shilingi Bilioni 73 umefikia 52% ya utekelezaji huku ukitarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025.
Kwa sasa kazi zinazofanyika ni kuweka tabaka la lami kilometa Saba, kujenga makalvati madogo na makubwa, kuweka tabaka la kokoto kilometa 9 na kuweka tabaka la udongo uliochanganywa na saruji kilometa 13.