TSH BIL 80 KUTOLEWA KWA WAKANDARASI-MAJI
DODOMA
Serikali kupitia wizara ya maji imetoa kiasi cha shilingi bilioni 80 kwa ajili ya kulipa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji nchini ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa haraka na kila Mtanzania apate maji safi na salama.
Aidha serikali inaandaa mpango madhubuti na maalum wa kuwa na huduma ya maji safi na maji taka katika vituo vyote vya afya, zahanati pamoja na shule ambazo hazijapata huduma hizo.
Maandalizi ya mpango huu yanatarajiwa kuanza Desemba 2024, ambapo utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuanza mara moja na utakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu na Katika kufikia lengo hilo, Serikali hadi sasa imewezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa zahanati zipatazo 4,939 kati ya 6,134, kupitia miradi tofauti ukiwemo mradi mkubwa wa Ziwa Victoria.